Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nigeria yasaidia watu wake kupitia WFP

Nigeria yasaidia watu wake kupitia WFP

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limekaribisha msaada wa tani 5000 za mchele kutoka kwa serikali ya Nigeria.

Shirika hilo linasema mchele huo utasaidia kulisha karibu watu nusu milioni wakimbizi wa ndani katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo ililoghubikwa na machafuko na ambako tishio la baa la njaa ni kubwa.

WFP tayari imeshaanza kusambaza awamu ya kwanza ya mchele huo wa msaada na inatarajia kupokea tani zingine 2000 za ulezi zilizoahidiwa na serikali ya Nigeria.

Photo Credit
Picha:WFP_Nigeria