Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yakaribisha mchango wa dola milioni 1 kwa ajili ya wakimbizi wa Sahrawi

WFP yakaribisha mchango wa dola milioni 1 kwa ajili ya wakimbizi wa Sahrawi

Pakua

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limekaribisha mchango wa dola milioni moja kutoka Marekani kwa ajili ya kusaidia wakimbizi walioko hatarini katika Mashariki mwa jangwa la Sahara nchini Algeria.

Kwa takriban miaka 40, wakimbizi wa mzozo wa muongo mmoja wa eneo lililoko katikati ya Morocco wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu Kusini Mashariki mwa Algeria.

WFP imesema itatumia fedha hizo kwa ajili ya kutoa msaada wa chakula kwa maelfu ya familia huku likiongeza kuwa usaidizi wa dharura unahitajikwa kwa ajili ya wakimbizi wa Sahrawi kwani wao hutegemea kwa kiasi kikubwa mgao wa chakula kwa ajili ya mahitaji ya chakula cha familia zao.

WFP imekuwa ikisaidi wakimbizi kutoka Mashariki mwa jangwa la Sahara nchini Algeria tangu 1986.

Photo Credit
UN Photo/Evan Schneider