Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICRC yaalani mauaji ya watoa huduma wa msalaba mwekundu CAR

ICRC yaalani mauaji ya watoa huduma wa msalaba mwekundu CAR

Pakua

Shirika la Kimataifa la Hilali Nyekundu na Msalaba Mwekundu, ICRC, limeelezea kusikitishwa na vifo vya kikatili vya wafanyakazi wa kujitolea wa msalaba mwekundu nchini Jamhuri ya Afrika ya kati, CAR wiki hii.

Kwa mujibu wa taarifa, wafanyakazi hao walikuwa kwenye mkutano wa dharura katika kituo cha afya cha Gambo, Mbomou Kusini mashariki mwa CAR mnamo Agosti 3 ambako ripoti zinaonyesha kwamba raia na watoa huduma wa afya huenda pia waliuwawa.

ICRC imeeleza hofu yake kuhusu kuibuka upya kwa machafuko nchini CAR katika miezi ya hivi majuzi,na kulenga kwa makusudi wafanyakazi wa kibindamu ambako kunasababisha watoa huduma kushindwa kusaidia jamii ambazo zimeathirika na mzozo.

ICRC imetuma salamu za rambi rambi kwa familia za wahanga na wafanyakazi wenza nchini CAR. Aidha wametoa wito kwa pande kinzani kuheshimu na kulinda watoa huduma za afya, vituo vya afya na kuwezesha usafirishaji wa wagonjwa na majeruhi kwa ajili ya kupata huduma za afya.

Shambulio kama hilo lililosababisha vifo vya wafanya kazi wa msalaba mwekundu ni la tatu mwaka huu.

Photo Credit
Picha:UNDOF