Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlipuko wa kipindupindu Sudan Kusini kuwa mbaya zaidi:IOM

Mlipuko wa kipindupindu Sudan Kusini kuwa mbaya zaidi:IOM

Pakua

Mlipuko wa kipindupindu Sudan Kusini unatarajiwa kuwa mbya zaidi wakati msimu wa mvua ukiendelea limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM. Onyo hilo limekuja wakati kuna mgogoro mkubwa wa kibinadamu uliosababishwa na miaka ya vita na kutawanywa kuliko athari mamilioni ya watu.

Zaidi ya visa 18,000 vya kipindupindu vimerekodiwa na karibu watu 330 wamepoteza maisha katika mlipuko wa karibuni tangu katikati ya mwezi Juni. Asilimia 60 ya nchi hiyo sasa haifikiki kutokana na mvua. Kwa mujibu wa Olivia Headon msemaji wa IOM Geneva, eneo la karibu na mto Nile ndilo lililoathirika zaidi , na ameongeza kuwa wanachofahamu ni kwamba hali itakuwa mbaya zaidi katika kipindi hiki.

IOM inasema hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo ni muhimu sana ili kudhibiti kuendelea kusambaa kwa ugonjwa huo uliodumu nchini Sudan Kusini kwa zaidi ya mwaka sasa.

Photo Credit
Rais akipatiwa chanjo ya kipindupindu kambini Sudan Kusini. Picha na WHO