Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfuko wa UM wasaidia tiba ya majeruhi wa shambulio la msikitini Afghanistan

Mfuko wa UM wasaidia tiba ya majeruhi wa shambulio la msikitini Afghanistan

Pakua

Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa msaada wa masuala ya kibinadamu umetenga dola 35,000 kwa ajili ya hospitali nchini Afghanistan inayotibu waathirika wa shambulio la kigaidi la msikitini umesema leo Umoja wa Mataifa.

Fedha hizo zimekabidhiwa kwa hospitali kuu ya Herat iliyoko Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo ambako takriban watu 44 waliuawa katika shambulio dhidi ya msikiti wa Kishia jumanne jioni.

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Toby Lanzer amesema msaada huo utasaidia hospitali kutoa huduma za dharura na wagonjwa mahtuti baada ya shambulio hilo.

Shambulio hilo limelaaniwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye pia ameelezea mshikamano na watu na serikali ya Afghanistan.

Photo Credit
Ali Ahmed, mmoja wa majeruhi aliyekuwa akisali msikitini, yuko katika hospitali wa Herat's nchini Afghanistan. Picha: UNAMA