Vijana washirikishwe katika kutimiza SDGs: Sauli

Vijana washirikishwe katika kutimiza SDGs: Sauli

Pakua

Umoja wa Mataifa unaendelelea kupigia chepuo ushirikishwaji wa vijana katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Malengo hayo ni mtambuka ambapo vijana wana nafasi kubwa ya kuyafanikisha malengo yote iwapo watapewa fursa. Katika mahojiano na Joseph Msami wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kijana Sauli Paul Mwame wa kidato cha nne katika shule ya sekondari DCM Mvumi, Dodoma, ambaye aliwakilisha nchi yake Tanzania katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG's anaanza kwa kueleza hisia zake baada ya kuzungumza mbele ya hadhira ya kimataifa kwa mara ya kwanza..

Photo Credit
Saul Paul Mwame akihutubia kikao cha Baraza Kuu jijini New York.(Picha:UM/Eskinder Debebe)