Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Urafiki unaweza kutumika kwa ajili ya mustakabali bora wa dunia-UM

Urafiki unaweza kutumika kwa ajili ya mustakabali bora wa dunia-UM

Pakua

[caption id="attachment_259999" align="alignleft" width="350"]overnightsaturday

Leo Julai 29 ni siku ya urafiki duniani, Umoja wa Mataifa katika ujumbe wake siku hii umesema, wakati dunia inakabiliana na changamoto, majanga na migawanyiko kama vile: umasikini, mizozo na ukiukwaji wa haki za bindamu miongoni mwa mambo mengine yanayozorotesha amani, usalama, maendeleo na muungano wa kijamii miongoni mwa watu, urafiki huenda ndio muaorobaini.

Katika kukabiliana na majanga na changamoto, ni lazima mizizi ya sababu iangaziwe kwa kuchagiza na kulinda umoja katika utu ambao unachukua sura nyingi ikiwemo urafiki.

Umoja huo umesema kwamba kupitia urafiki, kwa kujenga undugu na kuimarisha ushirikiano wa dhati, kuna uwezekano wa kuchangia katika kuleta mabadiliko yanayohitajika ili kuwa na utulivu wa kudumu, kuweka mazingira ambayo yatatulinda wote na kuimarisha ari kwa ajili ya dunia bora ambako watu wanaungana kwa ajili ya mustakabali mzuri kwa wote.

Photo Credit