UNMISS imejenga mahabusu ya kwanza ya wasichana Sudan Kusini

UNMISS imejenga mahabusu ya kwanza ya wasichana Sudan Kusini

Pakua

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umejenga mahabusu ya kwanza ya aina yake ya wasicha nchini humo.

Mahabusu hiyo Wau Juvenile Detention Centre ilikabidhiwa kwa serikali ili kuruhusu wasichana wahalifu kushikiliwa hapo na kesi zao kusikilizwa sambamba na vijana wenzao. UNMISS inasema ujenzi wa kituo hicho umegharimu dola za Marekani 35,000 na umechukua miezi miwli na nusu kukamilika.

Hivi sasa wasichana wadogo wanawekwa katika jela moja na wanawake watu wazima jambo ambalo linaathiri maendeleo yao kisaikolojia. Luteni Fidelia Massimino ni naibu mkurugenzi wa kituo hicho cha kurekebisha tabia , na anasema amefurahi kwamba sasa wana mahali pa kuwaweka wasichana na kurejkebisha tabia zao.

(SAUTI YA FIDELIA)

"Wasichana hawa watakaa nasi na tutawaangalia, na tunahisi kwamba tutawarekebisha tabia na kuwajumuisha tena kwenye jamii kwa usalama na pia washirikiana na jamii.”

Naye Erasmus Migyikra afisa wa ulinzi wa watoto wa UNMISS anasema..

(SAUTI MIGYKRA)

"Hivyo tunatarajia UNMISS, mashirika ya Umoja wa Mataifa, asasi za kiraia na serekali yenyewe wataungana ili kwamba tukamilishe wawe na shule ya mafunzo ya ufundi, wawe na shule za kawaida na vitu vingine ambavyo vitasaidia kuwabadilisha kama nyumbani, ili wasichana hao sio tu watasalia hapa na kusoma lakini pia waendelee kujifunza ujuzi mwingine ili waweze kujumuika vyema kwenye jamii.

Photo Credit
Mahakama ya watoto nchini Sudan Kusini. Picha: UM.Video capture