Skip to main content

Mtoto 1 kati ya 2 wanaokimbia Afrika hawataki kwenda Ulaya:UNICEF

Mtoto 1 kati ya 2 wanaokimbia Afrika hawataki kwenda Ulaya:UNICEF

Pakua

Watoto wengi walio safarini kutoka Libya kwenda Italia wamekimbia machafuko na hawakutaka kwenda Ulaya walipoondoka makwao umesema leo Umoja wa Mataifa.

Libya kwa muda mrefu imekuwa sumaku ya kuwanasa wahamiaji wanaotafuta kazi , lakini megene ya wasafirishaji haramu wa binadamu yameshika hatamu tangu kuenguliwa kwa Rais Muammar Ghadaffi 2011.

Shirika la Umoja wa mataiofa la kuhudumia watoto UNICEF leo limesema mjini Geneva Uswis kwamba karibu nusu ya vijana wadogo waliozungumza nao kwa ajili wamesema walitekwa kwa ajili ya kulipa fidia katika taifa hilo la Afrika ya Kaskazini lililosambaratishwa na vita.

Kwa wengi wao chaguo pekee walilonalo ni kuchukua safari ya hatari kwenye vyombo visivyofaa katika bahari ya Mediterranea. Sarah Crowe ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA SARAH)

“Wako tayari kuchukua safari hizi za hatari kwa sababu ya kilichowapata Libya. Kama kijana mmoja mdogo kutoka Gambia alivyoniambia hivi karibuni , kama una simba nyuma yako na bahari mbele yako , utachagua bahari.”

Wengi wa viajana waliohojiwa nchini Italia wametoka nchi za kusini mwa jangwa la sahara. Ukatili majumbani ulitajwa kama moja ya sababu kubwa za wao kuondoka, lakini wengi walielekeza lawama kwa kunyimwa haki na pia vita.

Msichana mmoja kati ya watano pia walisema ndoa za utotoni ilikuwa chachu ya wao kukimbia. Nchini Italia watoto waliowasili bila wazazi au walezi idadi yao imekuwa mara tatu kutoka mwaka 2012 hadi 2016 na kufikia karibu watoto 26,000.

Photo Credit
Wakimbizi na wahamiaji wakisubiri kushuka kutoka meli ya wanamaji ya Italia ili waingie kwenye meli nyingine itakayowafikisha mji wa Pozallo. (Picha:UNHCR/Francesco Malavolta)