Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua mafunzo ya kitaifa ya mitaala ya mahakama Somalia

UM wazindua mafunzo ya kitaifa ya mitaala ya mahakama Somalia

Pakua

Serikali ya shirikisho ya Somalia kwa pamoja na Umoja wa Matafia wamezindua programu ya kutoa mafunzo kwa maafisa wa sheria takriban 350 kote nchini katika juhudi za kusaidia kujenga upya mamlaka ya mahakama nchini humo.

Akizindua programu hiyo, mwanasheria mkuu wa Somalia Ibrahim Idle Suleyman amesema mfululizo wa mafunzo utasaidia katika kuleta mabadiliko ya kisheria na kuendeleza sheria ili kufikisha nchi hiyo katika kiwango cha kimataifa.

Bwana Suleyman ameongeza kwamba muundo wa kisiasa umebadilika na kuleta athari kwa mahakama na hivyo ni muhimu kuleta mabadikiliko kwenye mahakama pia.

Programu hiyo imewezeshwa kwa ushirikiano shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, ujumbe wa Umoja wa Mataifa Somalia, UNSOM, Muungano wa Ulaya, idara ya maendeleo ya kimataifa ya Uingereza na wanachama wa kitengo cha sheria chuo kikuu cha Mogadishu.

Photo Credit
Picha:UNSOM