M-pesa yaokoa waathirika wa ukame, Kenya

M-pesa yaokoa waathirika wa ukame, Kenya

Pakua

Mpango wa kuhamisha fedha kwa tekinolojia ya simu za rununu umesaidia waathirka wa ukame zaidi ya 250,000 kuepuka njaa iliokithiri nchini Kenya, kando na kufikia mahitaji mengine mengi ya kila siku, limesema Shirka la Msalaba Mwekundu nchini Kenya (KRCS).

Katika miezi mitatu iliopita, Shirika hilo limetoa shilingi za Kenya 3,000 za msaada wa kila mwezi, kwa kila familia kwa zadi ya familia 41,000 zilizoathriwa na ukame katika kaunti 13.

Katibu Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini humo, Dr Abbas Gullet, amesema mpango wa kuhamisha fedha (M-Pesa) umerahishisha uitikio wao kwa dharura hasa katika maeneo ya mashinani, fursa nadra katika shughuli za kibinadamu.

Kulingana na tathimini ya shirika hilo zaidi ya asilimia 60 ya familia zinazopokea msaada kwa M-Pesa zinaweza kupata milo mitatu au miwili kwa siku ikilinganishwa na asilimia 20 kabla ya kuanzisha muitikio kwa M-Pesa, katika nchi hiyo ambako watu million 3.5 wanakadiriwa kuhitaji msaada wa chakula kwa dharura.

Photo Credit
M-pesa.(Picha:Video capture/World Bank)