Watu milioni 1.7 Sudan Kusini hataraini kukumbwa na njaa

Watu milioni 1.7 Sudan Kusini hataraini kukumbwa na njaa

Pakua

Takribani watu milioni mbili nchini Sudan Kusini wako hatarini kukumbwa na njaa kali licha ya tangazo la hivi karibuni kuwa njaa si tishio tena katika baadhi ya maeneo nchini humo.

Onyo hilo limetolewa na shirikisho la msalaba mwekundu duniani, IFRC, shirika ambalo ni mdau wa Umoja wa Mataifa, wakati huu ambapo mzozo unaendelea Sudan Kusini ikikaribia kuadhimisha miaka sita ya uhuru wake.

Mkuu wa operesheni za IFRC nchini Sudan Kusini Dkt. Michael Charles amesema ingawa suala la kwamba njaa imepatiwa suluhu baadhi ya maeneo, suala la janga la kibinadamu nchini humo lisisahaulike.

Amesema kando ya idadi hiyo ya watu walio hatarini kupata njaa, watu wengine milioni sita hawana uhakika wa chakula huku shida nyingine za magonjwa kama vile Malaria na surua zikiwanyemelea.

Photo Credit
Picha: UNMISS