Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mlango wa UNOCI kufungwa rasmi Juni 30

Mlango wa UNOCI kufungwa rasmi Juni 30

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amekaribisha hatua ya kufungwa rasmi kwa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Cote d’Ivoire (UNOCI) hapo kesho Juni 30 baada ya kupata mafanikio makubwa.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa , Guterres amepongeza juhudi za mpango huo na umakini wa kubadili ukurasa wa machafuko na vita na kuugeuza kuwa amani nchini humo.

Pia amewashukuru wadau wote wa kitaifa, kikanda na kimataifa kwa mchango wao mkubwa katika mchakato wa amani ya Cote d’Ivoire. Katibu mkuu ameshukuru pia kazi nzuri iliyofanywa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa UNOCI Cote d’Ivoire, Aïchatou Mindaoudou, na waliomtangulia , huku akiwashukuru wafanyakazi wote wa mpango huo askari na raia na pia kuwakumbuka walinda amani 150 waliopoteza maisha katika miaka 13 ya mpango wa UNOCI na kuzishukuru pia nchi zote zilizochangia walinda amani hao.

Photo Credit
Walinda amani wa UNOCI.(Picha:UNOCI/flickr)