Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaonya wakimbizi wa Nigeria wanaorejea makwao

UNHCR yaonya wakimbizi wa Nigeria wanaorejea makwao

Pakua

Umoja wa Mataifa umesikitishwa na taarifa kwamba idadi kubwa ya wakimbizi wa Nigeria waliohifadhiwa nchini Cameroon wanarejea Kaskazini mwa Nigeria huku kukiwa na hali tete isiyo rafiki kwa mapokezi ya wakimbizi hao.

Kamishina Mkuu wa shirika la umoja huo la wakimbizi UNHCR Filippo Grandi amenukuliwa akisema majuam matatu yaliyopita UNHCR ilionya kuhusu hali mbaya mpakani mwa Nigheria mjini Banki ambapo maelfu walikuwa wanarejea.

Amesema eneo hilo halina malazi, kuna watu wengi kupindukia, upungufu wa huduma za maji safi na kujisafi na hatari ya magonjwa itokanayo na msimu wa mvua unaokaribia kuanza.

Grandi ameonya kuwa hata kabla ya kurejea kwa kundi hilo, mji wa Banki ulikuwa mwenyeji wa wakimbizi wa ndani 45,000 na sasa wanigeria zaidi ya 800 wengi wao wakiwa watoto wamewasili na kusisitiza kuwa kurejea huko kusiwe endelevu.

Amesema UNHCR imeanza kuwapa taarifa wakimbizi hao wanaotoka kambi ifahamikayo kwa jina la Minawo nchini Cameroon, ili kuhakikisha kuwa wana uelewa wa kutosha wa hali tete ya kule wanakotaka kuelekea kabla ya kufanya uamuzi.

Photo Credit
Mkimbizi kutoka Nigeria aliyekimbilia Cameroon.(Picha:UNHCR/Alexis Huguet)