Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za UM akamilisha ziara DRC

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za UM akamilisha ziara DRC

Pakua

Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix, leo Ijumaa amekamilisha ziara yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Akiwa nchini humo amepata fursa ya kutembelea Goma mji mkuu wa jimbo la Kivu ya Kaskazini na kukutana na gavana wa jimbo hilo Julien Paluku na wawili hao wakajadili hali ya usalama, uhusiano baina ya jamii jimboni humo na pia kazi za mpango wa Umoja wa Mataifa DRC, ujulikanao kama MONUSCO.

Lacoix kisha akafunga safari kuelekea jimbo la Kasai ambalo linashuhudia machafuko baina ya vikosi vya serikali na makundi yenye silaha, machafuko yaliyokatili maisha ya mamia ya watu na kuwafungisha virago maelfu. Na leo mwisho wa ziara yake amekuwa na mkutano na viongozi wa serikali akiwemo Rais Joseph Kabila mjini Kinshasa.

Bwana Lacoix kwa niaba ya Umoja wa Mataifa ameahidi juhudi za kuwasaidia watu wa DRC hazitokoma

Photo Credit
Mkuu wa operesheni za ulinzi za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix alipokutana na gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini Julien Paluku.(Picha:MONUSCO/Myriam Asmani)