Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM sasa kusaidia wahamiaji kwa huduma za kibalozi mtandaoni

IOM sasa kusaidia wahamiaji kwa huduma za kibalozi mtandaoni

Pakua

Shirika la kimataifa la wahamiaji IOM limezindua huduma za kibalozi mtandaoni katika juhudi za kutekeleza mpango wa kurejea makwao kwa hiari, na huduma za kibinadamu za dharura kwa wahamiaji ( AVRR) walioko Libya waliokwama.

Kwa mujibu wa IOM, kwa mara ya kwanza mkutano wa huduma za ubalozi mtandaoni umefanyika mnamo Juni tano kupitia Skype kwa ushirikiano na ubalozi wa Ghana mjini Tripoli nchini Libya.

Huduma hii huwaunganisha mtandaoni, mhamiaji kwa wawakilishi wa ubalozi wake, ili apokee taarifa muhimu kabla ya kupatiwa usaidizi wa huduma ya AVRR.

Mathalani wakati wa huduma hiyo kwa mara ya kwanza, mhamiaji mmoja wa Ghana aliyekuwa katika kizuizi kiitwacho Shahat, kilichoko kilometa 250 kutoka Benghazi, Libya, alipokea hati zake za kusafiria.

Photo Credit
IOM sasa kusaidia wahamiaji kwa huduma za kibalozi mtandaoni.(Picha:IOM)