IAEA yakusanya wabobezi kubongoa bongo kukabiliana na saratani

IAEA yakusanya wabobezi kubongoa bongo kukabiliana na saratani

Pakua

Wataalamu wa afya zaidi ya 500 kutoka nchi 96 watakutana kwa siku tatu kubongoa bongo kuhusu namna ya kutumia mionzi ya atomiki katika kutibu saratani.

Taarifa ya shirika la kimataifa la nguvu za Atomiki AEA imesema kwamba kuanzia tarehe 20 hadi 23 Juni, mjini Vienna nchini Austria, watalaamu hao watajikita katika kujumuisha jukumu la tiba mionzi hiyo dhidi ya kansa katika kukabiliana na ongezeko la saratani duniani.

Saratani ni moja ya magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo duniani na tiba ya mionzi ni miongoni mwa tiba muhimu na bei nafuu kwa aina nyingi za saratani.

Mkutano huo utasikiliza mada na kushuhudia kazi za wataalamu waliobobea katika masuala ya tiba ya saratani.

Photo Credit
Picha:IAEA