Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya vifo vya raia Syria inasikitisha-Pinheiro

Idadi ya vifo vya raia Syria inasikitisha-Pinheiro

Pakua

[caption id="attachment_257435" align="alignleft" width="350"]hapanapalepinheiro

Mgogoro nchini Syria unaendelea kusababisha madahara makubwa kwa raia ambao wanabeba gharama kubwa ya vita vilivyodumu kwa zaidia ya miaka sita sasa amesema mkuu wa tume ya uchunguzi kwa ajili ya Syria.

Akitoa taarifa ya maendeleo kwenye baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswis jumatano ,Paulo Pinheiro,mwenyekiti wa tume hiyo ya uchunguzi ametoa wito kwa pande kinzani kusitisha mapigano na kurejea kwenye meza ya mazungumzo, kwani tangu kuanza kwa machafuko baina ya majeshi ya serikali na wanamgambo wa upinzani maelfu kwa maelfu ya raia wamepoteza maisha na mamilioni kuzikimbia nyumba zao.

(SAUTI YA PINHEIRO)

“Kila wakati, pande kizani nan chi zenye ushawishi zimeshindwa kutumia fursa inayotolewa ili kukomesha uhasama. Na kila wakati wanaume, wanawake na watoto wa Syria ndio wanaolipa gharama ya kuendelea kwa vita hivyo. Pande kinzani ni lazima zihakikishe hazipitwi na fursa nyingine.”

Photo Credit