Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna matumaini, japo kibarua bado kipo kukomesha ukatili dhidi ya albino:Ero

Kuna matumaini, japo kibarua bado kipo kukomesha ukatili dhidi ya albino:Ero

Pakua

Kuna kila sababu ya kuwa na matumaini katika kuhakikisha ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi unakomeshwa hususani Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ambako tatizo hili limemea mizizi.

Hayo ni kwa mujibu wa Ikponwosa Ero mtaalamu huru wa haki za binadamu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi au albino akizungumza na Idhaa hii katika siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu ulemavu wa ngozi ambayo huadhimishwa kila mwaka Juni 13.

Bi ero amesema utashi wa kisiasa wa viongozi na mkakati wa kuchukua hatua wa Afrika vinatoa nuru

(SAUTI YA ERO 1)

“Matumaini yapo katika mpango huu wa hatua wa kikanda ambao niliuanzisha kwa kushirikiana na wadau mbalimbali barani kote kuanzia mashinani, makundi ya asasi za kiraia hadi mashirika ya maendeleo ya kimataifa, kwa hiyo tunafurahi na kujivunia kwamba hii ni suluhu ya Afrika kwa kile kinachoonekana kuwa tatizo la Afrika hasa kuhusu mashambulizi”

Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘kusonga mbele kwa matumaini mapya” hata hivyo Bi ero amesema bado kuna changamoto

(SAUTI YA IKPONWOSA ERO )

“Changamoto kubwa ni utekelezaji,hasa linapokuja suala la haki za binadamu katika kanda, hata kama kuna utashi wa kisiasa baadhi ya nchi zinafanya vizuri lakini nyingi zinasuasua kwa sababu mbalimbali,kupata rasilimali na kuziratibu jinsi ya kutumika katika kutekeleza mpango wa hatua wa kikanda.”

Photo Credit
Haki za albino. Picha: UNHRC