Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hifadhi kwa wanawake wahanga sio hiari-Šimonoviæ.

Hifadhi kwa wanawake wahanga sio hiari-Šimonoviæ.

Pakua

Nchi zinapaswa kuwapatia hifadhi ya malazi wanawake ambao ni wahanga wa vitendo vya ukatili kulingana na sheria ya haki za binadamu, amesema leo Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Dubravka Šimonoviæ.

Mtaalamu huru huyo ameliambia baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswisi wakati akiwasilisha ripoti yake, kuwa amri ya malazi na ulinzi ni zana muhimu za maisha zinazotoa ulinzi kwa wanawake wanaoshi katika mazingira hatarishi.

Hatua hizi sio hiari, ni wajibu wa haki za binadamu ambao ni muhimu katika kuhakikisha usalama wa wanawake na haki za binadamu, amesema Bi Šimonoviæ na kuongeza kuwa mataifa mengi hayana uelewa kuhusu wajibu wao wa kukabiliana na ukatili wa kijinsia ambao hujumuisha huduma hizo.

Amesema baadhi ya nchi zilikuwa hazina malazi huku nyingine zikiwa na vituo vya siku pekee ambavo havina uwezo wa kulaza wahanga.

Amependekeza kuwa katika makazi 10,000 kuwe na sehemu moja maalum ya hifadhi ya mkimbizi.

Photo Credit
Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili dhidi ya wanawake Dubravka Šimonoviæ akihutubia mkutano wa 61 wa tume kuhusu hali ya wanawake CSW hapo machi 2017 jijini New York. Picha: UM/Rick Bajornas