Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres alaani vikali shambulio la kigaidi Misri

Guterres alaani vikali shambulio la kigaidi Misri

Pakua

[caption id="attachment_319249" align="aligncenter" width="625"]hapanapalemisrisg

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani shambulio la kigaidi lililofanyika Minya Misri leo ijumaa, akisema hakuna sababu yoyote ya kuhalalisha ukatili huo wa kutisha.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa, Katibu Mkuu ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wahanga wa shambulio hilo, serikali na watu wote wa Misri.

Pia amewatakia nafuu ya haraka majeruhi na kutumai kwamba wahusika wa unyama huo watabainika na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Photo Credit