Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwekeza katika amani sasa ni muhimu kuliko wakati wowote ule

Kuwekeza katika amani sasa ni muhimu kuliko wakati wowote ule

Pakua

Katika kuadhimisha Siku ya Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa, Umoja huo unawaenzi zaidi ya walinda amani 3,500 ambao wamepoteza maisha yao katika huduma ya amani tangu mwaka 1948.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guerres akisistiza katika ujumbe maalumu wa siku hii ambayo kila mwaka huadhimishwa Mei 29.

Amesema kila siku walinda amani wanasaidia kurejesha amani na utulivu katika maeneo yaliyoghubikwa na vita na kwamba

(SAUTI YA GUTERRES)

“Kujitoa kwao kunaimarisha azma yetu ya kuhakikisha kuwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaendelea kulinda raia walioko hatarini, kuchagiza haki za binadamu na utawala wa sheria,kuendeleza mazungumzo na kulinda mustakhbali bora katika maeneo wanakotumwa kuhudumu.”

Ameongeza kuwa ni muhimu dunia kushikamana ili kuhakikisha azma ya kuwa na dunia yenye amani na utulivu kwa wote sasa kuliko wakati mwingine wowote ule.

Photo Credit
walinda amani wa UNMISS, UNPOL wakishirikiana na UNMAS na UNDSS wakiendesha operesheni ya kukusanya silaha na vifaa vingine vilivyopigwa marufuku kwenye makazi ya ulinzi wa raia Juba.Picha na UNMISS