Licha ya changamoto vita dhidi ya Ebola vayendelea DRC: WHO

Licha ya changamoto vita dhidi ya Ebola vayendelea DRC: WHO

Pakua

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, juhudi zinaendelea kukabiliana na mlipuko wa Ebola Kaskazini mwa nchi hiyo. Hadi sasa watu wane kati ya visa 43 vilivyoripotiwa wamefariki dunia katika eneo la Likati, kwa mujibu wa shirika la afya ulimwenguni , WHO.

Dr Matshidiso Moeti ni mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa WHO

(SAUTI YA DR MOETI)

"Sasa hivi tuna maabara inayozungunga katika eneo hilo na tunataraji sasa itaweza kuthibitisha visa kama ni Ebola au hapana haraka zaidi katika eneo hilo la kijijini, tunaweza kuwatoa watu huko haraka ukizingatia matatizo ya miundombinu hakuna barabara na pindi unapokaribia eneo hilo , ilnabidi tuwe na ndege au helkopta ili kufikisha watu, dawa na vifaa, lakini imewezekana kuanza kufanyika haraka.”

Msemaji wa WHO Tarik Jasarevic amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kwamba wagonjwa wengine watano wanapatiwa matibabu katika kituo maalumu na watu Zaidi ya 400 waliokutana nao wamefikiwa , 54 kati yao watibitishwa kutokuwa na shuku baada ya uangalizi wa siku 21 wa kubaini Ebola.

Serikali ya DRC bado haijatangaza endapo ina nia ya kupeleka chanjo ya majaribio ya Ebola , lakini maadandalizi yanaendelea kuhakikisha kwamba chanjo hiyo inaweza kusafirishwa katika kiwango cha joto kinachohitajika cha chini ya nyuzi joto 80.

Photo Credit
Juhudi za kukabiliana na Ebola katika kituo cha huduma za afya hulo Likati nchini DRC. Picha: WHO