Maafisa Somalia wajadiliana melini namna ya kuukabili uharamia

Maafisa Somalia wajadiliana melini namna ya kuukabili uharamia

Pakua

Kikosi cha wanamaji cha Umoja wa Ulaya EU, kilichoko nchini Somalia, kimemwalika Waziri Mkuu wa nchi hiyo Hassan Ali Khayre katika meli maalum na kufanya naye mazungumzo ya kukuza ushirikiano baina ya EU na Somalia katika ulinzi wa rasilimali ya maji nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa ya ujumbe wa Muungano wa Afriak nchini Somalia AMISOM, mazungumzo baina ya pande hizo mbili yanatarajiwa kusongesha mbele juhudi za kukabiliana na uharamia katika pwani ya Somalia, kazi inayotekelezwa na EU, inayotumia meli za shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP.

Majadiliano hayo melini, yalijikita katika opereshsni hiyo ya kupinga uharamia, matukio ya hivi karibuni ya uharamia na namna Muungano wa Ulaya EU, unavyoweza kusaidia zaidi serikali ya Somalia ili ishike hatamu katika ulinzi majini.

Waziri Mkuu Khayre kadhalika alipata fursa ya kufanya utalii ndani ya meli hiyo iitwayo ESPS Galicia, itumikayo kukabiliana na uharamia.

Photo Credit
Mazungumzo ya kukuza ushirikiano baina ya EU na Somalia katika ulinzi wa rasilimali ya maji nchini humo. Picha: AMISOM