Waziri Somalia auawa kwa kupigwa risasi

Waziri Somalia auawa kwa kupigwa risasi

Pakua

Nchini Somalia mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa, Michael Keating ametuma rambirambi kufuatia kifo cha Waziri wa ujenzi Abbas Abdullahi Sheikh Siraji, kilichotokea baada ya kupigwa risasi kwa bahati mbaya na walinzi karibu na ikulu mjini Mogadishu.

Katika salamu zake kupitia mtandao wa Twitter, Bwana Keating amesema marehemu Siraji alikuwa kijana mwenye ari ya utendaji na aliwakilisha vyema mawazo ya vijana.

Naye Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi "Farmajo" Mohamed katika rambirambi zake amemwelezea Waziri huyo aliyeuawa kuwa alikuwa mzalendo na mwaminifu.

Marehemu Siraji ni miongoni mwa mawaziri waliochaguliwa baada ya Rais Farmajoo kushinda uchaguzi na waliapishwa tarehe 21 mwezi Machi mwaka huu.

Photo Credit
Michael Keating, Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Somalia.(Picha:UNSOM)