ILO yaasisi elimu mtandao kwa wakimbizi wa Syria

ILO yaasisi elimu mtandao kwa wakimbizi wa Syria

Pakua

Shirika la kazi duniani limezindua mpango wa elimu mtandao kwa wakimbizi wa Syria walioko Jordan, mpango unaoeleza haki na wajibu chini ya sheria ya kazi ya nchini humo.

Nats!

Ndivyo inavyoanza video katika wavuti wa ILO inayowafunza wakimbizi hao ili kurasimisha kazi zao nchini Jordan. Mafunzo hayo yanaeainisha manufaa yakufanya kazi kihalali kwa kupata vibali vya kazi pamoja na taratibu za kuvipata.

Mpango huo wa elimu mtandao uliobuniwa na kampuni iitwayo Knowledge Horizon inayoelezwa kubobea katika mausala hayo, kadhalika umewezeshwa na wizara ya kazi ya Jordan ambapo njia zitumikazo ni pamoja na mafunzo kwa njia ya video.

Shirika la kazi duniani linasema kuwa haki za wafanyakazi, ulinzi wa kijamii, usalama na afya kazini ni miongonui mwa mitaala inayotolewa.

Photo Credit
Picha:ILO/Syria