Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasaidia wahamiani 421 waliokwama Libya kurejea Afrika

IOM yasaidia wahamiani 421 waliokwama Libya kurejea Afrika

Pakua

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM , Ijumaa limewasaidia wahamiaji 253 wa Nigeria waliokuwa wamekwama nchini Libya , kurejea nyumbani.

Wahamiaji hao ni wanawake 148, wanaume 105, na watoto sita . Wengi wa wahamiaji hao (235) walikuwa wanashikiliwa mahabusu kwenye vituo vya trig as Seka na Abu Slim mjini Tripoli na waliosalia walikuwa wakiishi mitaani.

Tarehe 27 Aprilii wahamiaji wengine zaidi walisaidiwa kurejesha Gambia wakiwemo wanaume 164, wanawake 4 na watoto waliokuwa peke yao 20.

Ndege zilizowasafirisha kwa msaada wa IOM ziliondoka wiki hii mjini Tripoli na walipowasili walipokea msaada kutoka kwa wafanyakazi wa IOM huko.

Photo Credit
Wahamiaji wa Afrika waliokuwa wamekwama nchini Libya wasaidiwa kurudi kwao. Picha: IOM/Video capture