Kusini Mashariki mwa Asia waahidi kupambana na magonjwa yaliyosahaulika

Kusini Mashariki mwa Asia waahidi kupambana na magonjwa yaliyosahaulika

Pakua

[caption id="attachment_316431" align="aligncenter" width="615"]hapanapaleasia

Nchi za ukanda wa Kusini Mashariki mwa asia zimeahidi kuchapuza juhudi za kutokomeza na kudhibiti magonjwa yaliyosahaulika au NTD’s ifikapo mwaka 2020 limesema shirika la afya ulimwenguni WHO hii leo.

Yakiathiri watu bilioni moja magonjwa yaliyosahaulika ni maradhi yaliyosheheni katika maeneo ya tropiki baadhi yakiwa ni ukoma, malale, na vikope. Mpango wa kuchukua hatua umepitishwa na nchi wanachama katika mkutano wa ngazi ya mawaziri uliofanyika Jumatano mjini Jakarta Indonesia.

Kwa mujibu wa WHO magonjwa haya huathiri zaidi watu waliotengwa, na jamii zilizosahaulika zikiwafanya watu hao kutumbukia zaidi katika umasikini na maisha yaliyoghubikwa na ulemavu na unyanyapaa.

Hata hivyo WHO inasema nchi nyingi za ukanda huo zinakaribia kukomesha maradhi hayo.

Photo Credit