Mtandao ndio umeme wa karne ya 21: Jack Ma

Mtandao ndio umeme wa karne ya 21: Jack Ma

Pakua

Mwanzilishi wa kampuni maarufu ya kidijitali Alibaba na Mshauri Maalum kwa Vijana wa Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD, Jack Ma amesema mtandao ni muhimu kama umeme na kila mtu anapaswa kuwa na huduma hiyo.

Ma amesema hayo wakati wa kongamano la wiki ya biashara ya mtandaoni ambayo inaendelea Geneva, Uswisi, ambao umeleta pamoja wajasiriamali vijana, wanawake katika biashara na wajasiriamali katika mazingira magumu kujadili teknolojia na biashara ya mitandao kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Amesema amepokea fursa hii kama mshauri maalum kwa vijana wajasiriamali na biashara ndogo ndogo, kuhakikisha kila mtu anapata huduma ya mtandao, huduma ambayo itajenga ajira kwa kufungua viungo vya biashara ya kimataifa, hivyo akatoa wito

(Sauti ya Ma)

" Mtandao upewe umuhimu sawa na umuhimu uliopewa umeme karne iliyopita. Na kila kitu kitakuwa mtandaoni na kila kilicho mtandaoni kitakuwa na taarifa. Na taarifa itakuwa nishati ya ufumbuzi."

Photo Credit
Jack Ma (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa UNCTAD Dkt. Mukhisa (kulia). Picha:UNCTAD