Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wabunge wanawake Somalia wanolewa

Wabunge wanawake Somalia wanolewa

Pakua

Wabunge wanawake nchini Somalia wamekutana kwa siku mbili mjini Mogadishu, na kuhitimisha mkutano huo leo kwa wito kwa wabunge hao kuungana katika kutia shime ajenda yao katika nyanja tofauti nchini humo.

Kwa mujibu wa ujumbe wa Muungano wa Afrika nchini humo AMISOM, Waziri wa wanawake na haki za binadamu Deeqa Yasin Yusuf, aliyefungua mkutano huo, uliowaleta pamoja wabunge wanawake kote nchini Somalia, amewataka wajfunze kufanya kazi pamoja ili kutimiza malengo.

Bi Yusuf amesema kuungana kutasaidia sauti za wanawake wabunge kusikika kila kona ya nchi.

Kwa upande wake spika wa bunge, Mohamed Sheikh Osman Jawari, amewataka wanawake kusaka mafunzo ya uongozi kupitia vyombo mbalimbali vya bunge ili kunoa ujuzi wao akisema kuwa uwezo wa wanawake katika uongozi iwe katika bunge, asasi za kiraia au mamlaka za juu unategemea mafunzo ili kukuza sifa za uongozi na kutatua changamoto za wanawake.

Photo Credit
Wabunge wanawake nchini Somalia wakutana mjini Mogadishu. Picha: UNSOM