Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lishe duni na utipwatipwa vyachangia hasara ya mabilioni Amerika ya Kusini - ripoti

Lishe duni na utipwatipwa vyachangia hasara ya mabilioni Amerika ya Kusini - ripoti

Pakua

Athari za lishe duni na uzito uliokithiri au utipwatipwa, zilichangia hasara ya mabilioni ya dola kwa uchumi wa nchi za Amerika ya Kusini, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotoewa leo na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP).

Ripoti hiyo ya utafiti uitwao “Gharama ya mzigo maradufu wa lishe mbovu: athari za kijamii na kiuchumi,” imebaini kuwa lishe mbovu – ambayo inajumuisha lishe duni na utipwatipwa – inachangia magonjwa na vifo, inaathiri matokeo ya elimu na uzalishaji, na hivyo kuwa na madhara makubwa ya kiuchumi kwa watu walioathiriwa, jamii zao, na nchi zao.

Kwa mujibu wa utaifiti huo, mazao ya jumla ya kila nchi hupungua kila mwaka, kutokana na hasara katika uzalishaji inayotokana na mzigo huu unaoibuka maradufu.

Hasara hii inakadiriwa kuwa dola milioni 500 nchini Chile, dola bilioni 4.3 nchini Ecuador na dola bilioni 28.8 nchini Mexico kila mwaka.

Photo Credit
Lishe duni na utipwatipwa vyachangia hasara ya mabilioni Amerika ya Latino. Picha: WFP/photo library