Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huku Somalia ikikumbana na ukame, watoto wakabiliwa na tishio la surua

Huku Somalia ikikumbana na ukame, watoto wakabiliwa na tishio la surua

Pakua

Takriban watoto 30,000 nchini Somalia wanapewa chanjo dhidi ya surua wiki hii, katika kampeni ya dharura huko Baidoa, mji wa Somalia ulioathiriwa zaidi na ukame. Wengi wa watoto hao ni wale waliolazimika kuhama makwao kutokana na ukame.

Kampeni hiyo inaongozwa na Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa (UNICEF) kwa ushirikiano na wadau wake.

Wengi wa watoto hao hawajawahi kupewa chanjo, kwani wametoka maeneo ya pambezoni ambayo ni vigumu wahudumu wa afya kuyafikia kwa sababu ya mgogoro uliolitatiza taifa hilo kwa miaka mingi.

Mwaka huu, takriban visa 5,700 vinavyoshukiwa kuwa vya surua vimeripotiwa nchini Somalia kufikia sasa, ikiwa ni zaidi ya idadi nzima iliyoripotiwa mwaka 2016.

Photo Credit
Wanawake waliofurushwa Baidoa wakiwa mjini Baidoa.(Picha:UN News/Laura Gelbert)