Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jinsia na uchumi vyamulikwa kwenye jopo Washington DC

Jinsia na uchumi vyamulikwa kwenye jopo Washington DC

Pakua

Ingawa faida za kuwawezesha wanawake kiuchumi na sera zinazochangia kuendeleza uwezeshaji huu zinajulikana vyema, bado kuna kazi nyingi ya kufanya ili kuweza kutimiza lengo la kuleta mabadiliko muhimu na ya muda mrefu.

Hayo yameibuka kwenye jopo lililoandaliwa na Shirika la Fedha Duniani, IMF na kampuni ya habari ya CNBC, katika mji mkuu wa Marekani, Washington DC. Dhima ya mjadala wa jopo hilo ilikuwa jinsia na uchumi, na hatua zinazopaswa kuchukuliwa siku za usoni.

Wanajopo hilo walijadili hatua zinazotakiwa kuchukuliwa, pamoja na kinachowezekana na kisichowezekana, na jinsi kila mdau, mathalani serikali, sekta binafsi na wengineo wanavyoweza kuchangia mabadiliko.

Photo Credit
Jopo lililoandaliwa na IMF na kampuni ya habari ya CNBC, katika mji mkuu wa Marekani, Washington DC.(Picha:UNifeed/video capture)