Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yasema chanjo ina umuhimu mkubwa zaidi kuliko inavyotambuliwa

WHO yasema chanjo ina umuhimu mkubwa zaidi kuliko inavyotambuliwa

Pakua

Wakati wiki ya chanjo duniani ikikaribia kung’oa nanga kuanzia Aprili 24 hadi 30, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa ingawa utoaji chanjo duniani ulizuia vifo milioni 10 kati ya mwaka 2010 na 2015, bado kuna watoto milioni 19.4 duniani ambao ama hawajapata chanjo au hawakupewa chanjo tosha.

WHO imesema kupitia chanjo, mamilioni ya watu pia walilindwa kutokana na uchungu na ulemavu unaotokana na ugonjwa kama numonia, kuhara, kifaduro, surua na polio.

Shirika hilo limesema programu fanisi za utoaji chanjo pia huwezesha kufanikisha masuala ya kipaumbele kitaifa, mathalan elimu na maendeleo ya kiuchumi.

Programu kuu ya utoaji chanjo iliasisiwa mnamo mwaka 1974, kutokana na ufanisi mkubwa na matumaini kuhusu uwezo wa dawa za chanjo, wakati ulimwengu ulipokaribia kutokomeza ndui.

Photo Credit
Picha:PAHO/WHO