Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kongamo la vijana kuchagiza uhifadhi wa utamaduni laanza:UNESCO

Kongamo la vijana kuchagiza uhifadhi wa utamaduni laanza:UNESCO

Pakua

Vijana takribani 80 kutoka mataifa ya ukanda wa hariri wanashiriki kungamano la kimataifa nchini Uchina wiki hii ambalo linachagiza ubunifu na uhifadhi wa utamaduni. Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushirikiano wa shirika la Umoja wa mataifa la elimu sayansi na utamaduni UNESCO na manispaa mbili za China.

Malengo ya kongamano hilo yanajumuisha kuwapa vijana fursa ya kupaza sauti kueleza hofu zao na kushirikishwa katika kulinda na kuhifadhi urithi wao. Binadamu wamekuwa wakifanya biashara ya bidhaa, kubadilishana ujuzi na mawazo katika ukanda wa hariri ukiunganisha Mashariki na Magharibi kwa karne.

Mbali ya Uchina nchi nyingine za ukanda wa Hariri zinajumuisha Afghanistan, Iran na India.

Photo Credit
Kongamano la vijana lililofunguliwa leo nchini Uchina kujadili ubunifu na uhifadhi wa utamaduni. Picha :UNESCO