Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nimeshtushwa na mauaji mengine ya kutisha Aleppo-O’Brien

Nimeshtushwa na mauaji mengine ya kutisha Aleppo-O’Brien

Pakua

Nimeshtushwa sana na taarifa za mauji mengine ya kutisha yakihusisha raia kwenye mlipuko karibu na msafara wakati wakihamishwa kutoka maeneo yaliyozingirwa Aleppo ya miji ya Foah and Kefraya.

Hayo yamesemwa na mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura (OCHA) bwana Stephen O’Brien wakati akutuma salamu za rambirami kwa familia za waliopoteza maisha na waliojeruhiwa katika shambulio hilo.

Amesema wahusika wa shambulio hilo la kinyama la kiuoga wamedhihirisha kutokuwa na soni ya kuthamini uhai wa binadamu. Ameongeza kuwa sheria za kimataifa za kibinadamu ziko wazi, pande zote kinzani katika mzozo ni lazima ziheshimu, zilinde raia na kutofautisha baina ya walengwa wa kijeshi na raia.

Zoezi la kuhamisha raia ni sehemu ya makubaliano kuhusu maeneo manne yanayozingirwa ya miji ya Foah na Kefraya iliyoko Idlib, na Madaya na Zabadani iliyoko Damascus vijijini.

Photo Credit
Jengo lililoharibiwa mjini Aleppo, Syria.(Picha:OCHA/Gemma Connell/maktaba)