Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais Somalia aapa kuwaondoa Al-Shabaab Mogadishu

Rais Somalia aapa kuwaondoa Al-Shabaab Mogadishu

Pakua

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed maarufu kwa jina la ‘Farmaajo’ ameahidi kutowesha wanamgambo wa Al-Shabaab ambao hivi karibuni wameripotiwa kuendelea kuua na kujeruhi raia wasio na hatia kwenye mji mkuu Mogadishu.

Akizungumza wakati wa sherehe za miaka 57 ya jeshi la nchi hiyo SNA mjini Mogadishu, Rais Farmaajo amewataka wanajeshi watumie fursa ya onyo la serikali la hivi karibuni kwamba wanaojihusisha na vitendo vya kigaidi watakiona cha mtema kuni.

Tutawasaka kila walipo. Tutatumia mbinu tulizotumia zamani na tutaikomboa nchi kwa uwezo wa vikosi vyetu, amesema Rais huyo wakati wa hafla iliyohudhuriwa pia na maafisa wa serikali, wale wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na maafisa wa ujumbe wa Muugano wa Afrika nchini Somalia AMISOM na jumuiya ya kimataiafa.

Rais Farmaajo kadhalika ametambua juhudi za maafisa wa AMISOM na SAN ambao waliongoza mikakati na mashambulizi ya kukiondoa kikundi cha kigaidi cha Al Shabaab mjini Mogadishu mwaka 2011, operesheni ambayo amesema ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Photo Credit
Operesheni ya kukamata wafuasi wa Al Shabaab mjini Mogadishu nchini Somalia.(UM/Tobin Jones/maktaba)