Shambulio la kemikali Idlib limetokea angani:De Mistura

Shambulio la kemikali Idlib limetokea angani:De Mistura

Pakua

Shambulio baya na la kutisha la silaha za kemikali kwenye jimbo la Idlib Syria Jumanne limetokea angani amesema mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria Staffan de Mistura na kuongeza kwamba ni lazima kudai uwajibikaji kwa wahusika

(SAUTI YA DE MISTURA)

"Kilichotokea asubuhi ya leo ni cha kutisha , na tumekuwa tukihoji na nina uhakika Umoja wa Mataifa utahoji pia na nina uhakika kutakuwa na mkutano wa baraza la usalama kuhusu hili, ili kubaini waliohusika na uwajibikaji”

Duru zinasema watu wapatao 70 wameuawa katika shambulio hilo na wengine 500 kujeruhiwa wengine vibaya sana.

Photo Credit
Mjumbe maalum wa UM kuhusu Syria, Staffan de Mistura. (Picha:UN/Violaine Martin )