Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fuateni nyayo za China fungeni viwanda vya pembe za ndovu-UNEP

Fuateni nyayo za China fungeni viwanda vya pembe za ndovu-UNEP

Pakua

Likipongeza hatua ya serikali ya Uchina ya kufunga viwanda na maduda yanayouza bidhaa za pembe za ndovu , shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP limetoa wito kwa nchi na serikali kufuata nyayo za Uchina na kuboresha matuaini ya mustakhbali wa maisha ya ndovu kote duniani.

Hatua hiyo iliyotangazwa na uongozi wa misitu wa taifa hilo unawakilisha hatua ya kwanza madhubuti ya kukaribia kupiga marufuku kabisa biashaya ya pembe za ndovu nchini China. Uamuzi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa kikamilifu mwoishoni mwa mwaka 2017.

Mkurugenzi mtendaji wa UNEP Erik Solheim amesema hiyo ni hatua ya kihistoria na inaweza kuwa ndio pinduko la vita dhidi ya kuokoa maisha ya tembo wasitoweke kabisa. Ameongeza kuwa na kipimo cha hatua za mafanikio ya sheria hizo mpya itakuwa ni jinsi gani zitakavyotekelezwa ipasavyo.

Kwa mujibu wa UNEP kufungwa huko kwa viwanda na maduka hapo 31 Machi mwaka huu, kunaashiria kumalizika kwa biashara ya takribani theluthi moja ya bidhaa zitokanazo na pembe za ndovu katika moja ya soko kubwa kabisa duniani la pembe za ndovu, ambako pembe hizo hutumika kutengeneza mapambo na kutolewa zawadi au kunadi utajiri.

Tembo 100,000 wameuawa muongo uliopita pekee na tembo laki 5 ndio waliosalia duniani kote, hivyo UNEP inasema marufuku hiyo imekuja wakati muafaka.

Photo Credit
Ndovu ambao wanauwawa kwa ajili ya mauzo ya pembe zao.(Picha:UNEP)