Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imezindua mkakati wa kutokomeza njaa Zimbabwe

WFP imezindua mkakati wa kutokomeza njaa Zimbabwe

Pakua

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP kwa ushirikiano na serikali ya Zimbabwe, Jumatatu wamezindua mpango wa miaka mitano wa kujenga uhimili, kutokomeza njaa na kuboresha lishe nchini humo.

Mkakati huo mpya wa kuhakikisha Zimbabwe huru bila njaa, utaimarisha ushirika wa WFP na taifa hilo huku ukihakikisha Wazimbabwe wanajengewa uwezo hasa wasio jiweza kuwa na uhakika wa chakula amesema mwakilishi wa WFP nchini humo Eddie Rowe.

WFP ni shirika la kwanza la Umoja wa Mataifa kujipangia mkakati wake wa (2017-2021) sanjari na malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).

WFP inasema Zimbabwe, kuanzia Aprili Mosi, ni moja ya nchi za kwanza kutekeleza mkakati huo katika kiwango cha nchi. Mkakati huo unalenga katika kusaidia juhudi za muda mrefu za taifa katika masuala ya kijamii na kuimarisha mifumo na taasisi zinazohitajika ili kusaidia kufikia lengo la njaa sufuri.

Photo Credit
Nchini Zimbabwe WFP na shughuli za usambazaji chakula.(Picha:WFP/R. Lee)