Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wadhihirisha kuwa kazi ni kazi bora iwe halali

Wanawake wadhihirisha kuwa kazi ni kazi bora iwe halali

Pakua

Mkutano wa 61 wa kamisheni ya hali  ya wanawake duniani, CSW61 ukiendelea kushika kasi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, nchini Tanzania wanawake wa mashinani wameanza kuonyesha bayana kuwa zama za kazi fulani ni za wanaume na nyingine ni za kike zimepitwa na wakati. Mathalani udereva wa magari ya abiria, uwakala wa wasafiri na nyinginezo nyingi. Je ni wapi huko? Paulina Mpiwa wa radio washirika Sengerema FM mkoani Mwanza amevinjari wilayani Sengerema.

Photo Credit
Kazi ni kazi bora iwe halali na mkono uende kinywani. (Picha:UN/Peacekeepers)