Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sera zinazojali jinsia zimeleta mafanikio kwa kampuni- UNWomen

Sera zinazojali jinsia zimeleta mafanikio kwa kampuni- UNWomen

Pakua

Kampuni zinazoajiri wafanyakazi kwa kuzingatia sera za usawa wa kijinsia zimedhihirisha jinsi mwelekeo huo ulivyo na manufaa kwa maendeleo ya kampuni husika.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen Phumzile Mlambo-Ngucka amesema hayo akihojiwa na radio ya huo katika maadhimsisho ya siku ya wanawake duniani hii leo.

Amesema kampuni hizo zimeibuka kidedea dhidi ya kampuni nyingine katka tasnia sawa akisema..

(Sauti ya Phumzile)

“Mathalani kwenye tasnia ya ukaguzi, Ernst & Young imeonyesha kuwa iwapo ukituma kwa mteja wako timu ya ukaguzi yenye usawa wa kijinsia unamwacha mteja wako akiwa ameridhika. Na katika sekta nyingi na viwandani ubora wa uamuzi unaimarika pindi unapokuwa na timu jumuishi na siyo wanawake tu,bali pia watu wenye ulemavu, na makundi madogo.”

Kuhusu kile anachopenda kuona siku hii ikiadhimishwa, mkuu huyo wa UNWomen amesema..

(Sauti ya Phumzile)

Baadhi ya nchi zimechagua kusherehekea siku ya wanawake kwa kuhakisha wanawake hawatokuwepo kazini ili watu waone ni jinsi gani unaweza kumaliza siku bila mwanamke au mwanamke kutokuwepo kazini. Hii itakuwa jambo la kusubiria kuona nini kitatokea.”

Ujumbe wa mwaka huu ni wanawake katika mazingira ya ajira yanayobadili; mwelekeo 50-50 ifikapo mwaka 2030.

Photo Credit
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen Phumzile Mlambo-Ngucka nchini Sweden azungumza kuhusu uwezeshaji wa wanawake. Picha: UN Women