Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukarabati wa barabara inayounganisha DRC na Burundi waanza

Ukarabati wa barabara inayounganisha DRC na Burundi waanza

Pakua

Huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO umeanza ukarabati wa barabara inayounganisha jimbo la Kivu Kusini na Burundi kupitia Uvira.

Ukarabati wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa Sita utafanyika kwa siku 50 na hivyo kumaliza adha ya usafiri ambapo wananchi walitumia nusu saa kwa gari kusafiri kilometa moja.

Mkuu wa ofisi ya MONUSCO huko Uvira, Ould Mohamed Elhacen amesema barabara hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa pande mbili za nchi hiyo.

Mathalani amesema eneo la mpakani la Kavimvira ni muhimu kwa huduma za ushuru na uhamiaji kwa pande zote hiyo ukarabati utaimarisha biashara kati ya Burundi na DRC.

Photo Credit
Ukarabati wa barabara inayounganisha jimbo la Kivu Kusini na Burundi kupitia Uvira nchini DRC  hadi Kavimvira nchini Burundi umeanza leo. (Picha: MONUSCO)