Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani yatoa kanuni mpya za ukimbizi, UNHCR yasisitiza misingi ni ileile

Marekani yatoa kanuni mpya za ukimbizi, UNHCR yasisitiza misingi ni ileile

Pakua

Kufuatia amri mpya ya Marekani ilyotolewa leo kuhusu wanaosaka hifadhi ya ukimbizi nchini humo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesisitiza kuwa wakimbizi ni watu wa kawaida wanaokimbia vita, ghasia au mateso na bado wanasalia na umuhimu wa kupatiwa hifadhi na ulinzi.

Kamishna Mkuu wa UNHCR Filippo Grandi amesema nia inasalia ile ile ya kuwapatia ulinzi na kwamba hatua hii ya Marekani ingawa ni ya muda inaweza kuwa na madhara kwa wale ambao inawagusa.

Amesema kwa muda mrefu UNHCR imekuwa na ushirikiano na Marekani katika kusaka suluhu za wakimbizi na wanatarajia kuendelea kushirikiana kupatia suluhu wale wanaosaka hifadhi.

UNHCR imesisitiza kuwa iko tayari kujadiliana na serikali ya Marekani kuhakikisha mipango yote ya kuhudumia wakimbizi inakidhi vigezo vya hali ya juu kwa ajili ya ulinzi na usalama.

Photo Credit
Kamishna Mkuu wa UNHCR, Fillipo Grandi .(Picha:UM/Evan Schneider)