Skip to main content

Neno la Wiki - Si ndiyo

Neno la Wiki - Si ndiyo

Pakua

Katika neno la wiki Februari 3 tunachambua neno si ndiyo, mchambuzi wetu leo ni, Nuhu Zuberi Bakari ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa masuala ya mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA.

Bwana Nuhu anasema kuwa "si ndiyo" ni semi ambayo moja ni kikanushi na moja ni ya kukubali, hivyo mtu anapotumia maneno  yote mawili kumhakikishia mtu hakuna usanifu wowote. Bwana Bakari anasema mazoea na kasumba yanaharibu lugha. Matumizi sahihi ya kuhakikisha kauli ni kutumia ndiyo au hapana, sivyo au ndivyo. Sikiliza kwa kina maelekezo yake ili kuweza kunyoosha matumizi ya lugha sanifu na adhimu ya Kiswahili.

Photo Credit
Leo tunaangazia neno la wiki na neno hilo ni "si ndiyo" mchambuzi ni Nuhu Zubeir Bakari kutoka CHAKITA nchini Kenya. (Picha:Idhaa ya Kiswahili)