Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa maendeleo chanzo cha migogoro Nigeria: UNDP

Ukosefu wa maendeleo chanzo cha migogoro Nigeria: UNDP

Pakua

Mkutano wa jumuiya ya kimataifa wa kujadili jinsi ya kuongeza msaada kwa bonde la ziwa Chad ambako nchi za Cameroon, Chad, Niger na Nigeria ziko katika hatihati ya janga kubwa la kibinadamu, ukiwa umeanza leo, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP nchini Nigeria, limesema mipango ya kimaendeleo ya muda mrefu itasaidia mamailioni ya watu wanaohitaji msaada katika maeneo yanayoendelea kukombolewa kutoka kundi la kigaidi la Boko Haram

Katika mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa kutoka mjini Oslo, Mratibu Mkazi wa UNDP nchini humo Edward Kallon, amesema UNDP inakusudia kutumia mkakati wa mpango wa muda mrefu  katika kutoa usaudizi kwa wahitaji nchini Nigeria.

( Sauti Edward)

‘‘Tunachomaanisha hapa ni kujaribu kuhakikisha kwamba wakati mipango ya muda mfupi  inafikiwa, tunataka kuhakikisha kwamba mahitaji ya kati na muda mrefu yanashughulikiwa pia kupitia mkakati wa uwezo wa kurejelea maisha baada ya madhila.’’

Amesema ili kutekeleza hilo kinachojumuishwa ni.

(Sauti Edward)

Kushughulikia chanzo cha migogoro  ambacho kimsingi ni ukosefu wa maendeleo, madhara ya mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa haki za binadamu na utawala na pia kipato na kukosekana kwa usawa, na kwa kiwango fulani madhara ya kiitikadi.

Machafuko yakiwemo ya Boko Haram yamewafanya watu zaidi ya milioni 2.3 kuzihama nyumba zao huku milioni 7 wakikabiliwa na njaa. Utapia mlo uliokithiri unatishia maisha ya watoto zaidi ya nusu milioni huku jumla ya watu milioni 11 wakihitaji msaada wa harak

Photo Credit
Wakimbizi kutoka Nigeria nchini Chad. Picha:WFP West Africa