Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu akaribisha uamuzi wa Gambia kusalia uanachama ICC

Katibu Mkuu akaribisha uamuzi wa Gambia kusalia uanachama ICC

Pakua

[caption id="attachment_298924" align="alignleft" width="350"]gambiaicc

Tarehe 10 Februari ubalozi wa kudumu wa Gambia kwenye Umoja wa Mataifa uliwasilisha ujumbe kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusu kufuta uamuzi wa nchi hiyo kujiondoa kwenye mkataba wa Roma wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq , Gambia ilimjulisha rasmi Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kuhusu uamuzi wa kujitoa ICC tarehe 10 Novemba 2016, uamuzi ambao Katibu Mkuu alisikitishwa nao.

Taarifa hiyo inasema Gambia kama ilivyo mataifa mengi ya Afrika imekuwa na jukumu kubwa katika majadiliano yaliyosaidia kupitishwa kwa mkataba wa Roma , na ilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza zilizotia saini.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa hiyo leo Katibu Mkuu amekaribisha hatua ya Gambia kwamba itaendelea kusalia kama mwanachama wa mkataba huo wa Roma wa mahakama ya ICC na anaamini kwamba nchi wanachama wataendelea kuimarisha mahakama hiyo kupitia majadiliano.

Photo Credit