Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwekeza kwa vijana ni kuwekeza kwa taifa-Guterres

Kuwekeza kwa vijana ni kuwekeza kwa taifa-Guterres

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres yuko ziarani nchini Misri ambapo amesema nchi hiyo ni mchangiaji muhimu katika utatuzi wa matatizo mengi yanayoukumba ukanda huo kutokana na historia, utamaduni na mazingira yake ya kisiasa, akigusia suala la ugaidi na upokeaji wa wakimbizi.

Akizungumza katika chuo kikuu cha Cairo nchini humo amesema vijana wanamchango mkubwa katika kuhakikisha maendeleo ya taifa, utatuzi wa migogoro , kuleta amani na kudumisha usalama. Hata hivyo amesema mara nyingo kundi hilo husahaulika au halipewi kipaumbele kinachotakiwa

 (GUTERRES CUT 1)

“Taharuki inayotawala miongoni mwa vijana ambao hawana matumaini na mustakhbali wao ni chanzo kikubwa cha kutokuwepo usalama duniani, na ni muhimu wakati serikali zinapanga mikakati yao ya kiuchumi na wakati jumuiya ya kimataifa inaunda mifumo ya ushirikiano ni muhimu kuweka masuala ya ajira ya vijana, ujuzi kwa vijana katika kitovu cha kipaumbele chao, na kwa bahati mbaya mara nyingi hili husahaulika, na ili kuliepuka hilo ni bora kuwekeza katika kuwawezesha vijana”

image
Katibu Mkuu Guterres na viongozi wa Misri mjini Cairo: Picha na Ofisi ya Rais Misri
Katibu mkuu ambaye pia amekutana na viongozi wa serikali ya Misri na kujadili masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano baina ya Umoja wa Mataifa nan chi hiyo, awali alikuwa na mkutano na waandishi wa habari na suala la amani ya Mashariki ya Kati na hususani suluhu ya kudumu baina ya Israel na Palestina lilijitokeza naye akasem

(GUTERRES CUT 2)

“Kwanza kabisa kukiwa na makubaliano kwamba hakuna mpango mwingine kwa suluhu ya hali baina ya Israel na Palestina isipokuwa suluhu ya mataifa mawili , ni vyuema kwamba kila liwezekanalo lifanyike kulinda uwezekano wa suluhu ya mataifa mawili , na pili kuwe na utashi wa kuhakikisha kwamba vita dhidi ya ugaidi vitatekelezwa kwa dhamira ya dhati.”

Photo Credit
Katibu Mkuu Antonio Guterres akiwa Misri: Picha na Ofisi ya Rais Misri