Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani raia kujeruhiwa katika maandamano Iraq

UM walaani raia kujeruhiwa katika maandamano Iraq

Pakua

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq UNAMI umeeleza kusikitishwa kwake na kujeruhiwa kwa raia kufuatia maandamano ya hii leo mjini Baghdad ambapo miongoni mwa waliojeruhiwa ni maafisa wa vikosi vya usalama.

Katika taarifa yake, UNAMI imeeleza kutambua tamko la Waziri Mkuu Haider al Abadi kuhusu haki ya wananchi kufanya maandamano kwa amani na kutii sheria na wajibu wa serikali katika kulinda waandamanaji na usalama wa raia.

Taarifa ya ujumbe huo imeongeza kuwa haki ya uhuru wa maandamano ya amani ni msingi wa demokrasia na ni lazima kuheshimiwa na kulindwa na wananchi, Serikali, na vikosi vya usalama wakati wote na katika hali zote.

Wananchi wana haki ya kutoa maoni yao, kuomba mabadiliko  mageuzi na mabadiliko na sauti zao kusikika, lakini ni lazima kufanya hivyo kwa amani na kwa kufuata kamili sheria, imesema taarifa hiyo.

UNAMI imekaribisha kuanzishwa kwa taasisi aliyoitaja Waziri Mkuu Abadi ya uchunguzi wa umma kwa tukio la leo.

Photo Credit
Picha: UNAMI/Sanaa Kareem