Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFPA yatoa huduma za afya ya uzazi na kujisafi kwa wanawake Iraq

UNFPA yatoa huduma za afya ya uzazi na kujisafi kwa wanawake Iraq

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la  ididi ya watu UNFPA  na wadau, wanasaidia huduma za dharura kwa wanawake na wasichana mjini Mosul nchini Iraq, eneo ambalo linakabiliwa na machafuko.

Kwa mujibu wa UNFPA, kundi hilo ambalo halijapewa kipaumbele na lenye mahitaji maalum ya afya ya uzazi na ulinzi linakadiriwa kuwa  kati ya 138,000 hadi 220,000.

Likishirikiana na serikali ya Iraq, wadau wa kitaifa na kimataifa, shirika hilo la idadi ya watu linasaidia wanawake kulinda hadhi zao kwa kuwapatia vifurushi 30,000 vyenye huduma za usafi na kujisafi kama miswaki, sabuni, taulo za kike na nguo za ndani.  Misaada mingine ni huduma za afya ya uzazi kwa walio katika kipndi cha kujifungua pamoja na misaada ya kisaikolojia.

Ugawaji wa misaada hiyo ulilenga  wilaya za  Mashariki mwa Mosul ambazo  zimeshikiliwa tena na vikosi mabazo kwa mujibu wa UNFPA  zina mahitaji makubwa zaidi.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa, idadi ya watu wanoishi mjini Mosul, inakadiriwa kuwa kati ya 550,000 hadi 885,000.

Photo Credit
Picha: © UNICEF Iraq/2016/Khuzaie